Living Water Centre, Makuti Kawe: Nia Yetu | Dhumuni Letu | Huduma Yetu | Mawasiliano

Karibu LWC - Kawe

..imekua ni furaha ya moyo wangu kumtumikia Bwana Yesu Kristo, aliye Bwana na Mwokozi wa Maisha yangu. Neema zake, Fadhili zake, Ahadi zake za Uaminifu wake Mkuu juu ya maisha yangu, zimekua ni baraka tele zisizo na kipimo. Nakukaribisha ujumuike nasi katika huduma yetu ya Living Water Cetre - Kawe...

Karibu LWC - Kawe:

Asante kwa kutumia muda wako kutembelea tovuti yetu ya Living Water Centre, Makuti Kawe. Living Water Centre, Makuti, Kawe ni huduma ya Kikristo inayoongozwa na Mtumishi wa Mungu, Mtume Onesmo N. Ndegi. Kama Neno la Mungu lilivyo kama Maji ya Uzima, au Maji yaliyo hai, Living Water Centre imekua ikifikisha Habari njema za Yesu Kristo kwa mataifa na kuleta watu waliopotea kwa Yesu Kristo. Neema na Baraka za Mungu, zimetufunika na kweli tumeuona Mkono wake katika Maombi, na tumeshuhudia Watu wakifunguliwa kutoka katika vifungo mbali mbali vya Shetani na Nguvu za Giza, na kujumuika pamoja kama watu wamoja wanaompenda Mungu, tukimfanyia Shangwe kwa Nyimbo na Kuabudu, kumtumikia na kuiambia Dunia matendo yake makuu..

LWC Kawe: Sisi kama kanisa la Mungu, tunaamini na tunaowajibu mkubwa katika kuleta maisha mapya yenye makusudi yaliyokusudiwa na Mungu mwenyewe kwa Waaminio katika Familia, Mtu mmoja mmoja, Jumuia, miji na nchi kwa ujumla. Tunapenda ukweli kwamba, Mungu ni mwaminifu na ahadi zake ni za kweli, na amekusudia sisi kuwa Chumvi ya ulimwengu, na kupitia sisi, Watu watauona Mkono wake, na wataufurahia uhalisia wa wema wa Mungu siku zote za maisha yao. Karibu ujumuike nasi. Mungu Wetu na akubariki sana.

Neno La Mungu

 

Sisi kama kanisa la Mungu, tunaamini na tunaowajibu mkubwa katika kuleta maisha mapya yenye makusudi yaliyokusudiwa na Mungu mwenyewe kwa Waaminio katika Familia, Mtu mmoja mmoja, Jumuia, miji na nchi kwa ujumla. Tunaupenda ukweli kwamba, Mungu ni mwaminifu na ahadi zake ni za kweli, na amekusudia sisi kuwa Chumvi ya Ulimwengu.

Biblia Takatifu